karibu text

KARIBU computerdevicedr

MAUJANJA BLOG

Uwanja wako pekee wa kupata maujanja mbali mbali kuhusu computer/device yako katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza kwenye matumizi ya computer/device yako. tuachie Maoni kwa jambo linalokutatiza Usaidike



Wednesday 2 May 2018

NINI CHA KUFANYA KWA DISABLED IPHONE

Kutokana na maombi ya mdau mmoja wa computerdevicedr maujanja blog, leo naweletea maujanja nini cha kufanya endepo iphone yako imekua disabled.
ujumbe wenye muonekano wa namna hii kwenye iphone yako waweza kukupa sononeko kubwa mno na ukijue nini cha kufanya. chanzo cha jumbe kama hiyo kwenye iphone ni kuwa mtumiaji anakuwa amesahau password yaka ma kujaribu mara nyingi mpaka kupelekea simu kuwa disabled 
kwa hali ya kawaida apa tungesema picha limeisha maandishi matatu the end, lakini kutoka maujanja blog leo utafahamu ni namna gani utachomoka kwenye sononeko hili na kuokoa fuba ambalo ungekiacha kwa wataalaam.

Hatua za kufanya / maandalizi 
awali ya yote hakikisha una kumbuka vizuri apple ID yako. 
1. hakikisha una computer ya windows ama MAC
2. uwe umesha install ITUNE version mpya kabisa
3. uwe na internet stable (isiwe inakata kata)
4. uwe na bundle ya kutosha kuanzia 5gb ukiweza ata 10gb kwa uhakika

kitakacho fuata hapa baada ya kuhakiki vitu vyote viko sawa ni kuchomeka simu yako kwenye computer (lakini kwa mtindo wa recovery mode)
- kuifanya iphone yako recovery mode kuanzia iphone za mwanzo ama zile zote zenye (home button) uta chomeka cable kwenye simu yako alafu huku umeshika home button bila kuachia chomeka cable kwenye computer. hapo simu yako itaonekana kwenye kioo ikiwa na alama ya itune ikiashiria tayari iko recovery mode.
(Alama hii ya ITUNE inaweza kuwa tofauti kwa rangi hilo lisikuogopeshe bado upo sawa hiyo ni kutokana na model ama software ulionayo kwa iphone yako.)

mambo yote ya kiwa sawa upande wa computer yako program ya ITUME itaisoma simu na kutoa taarifa kwamba utaitaji kuifanyia restore/update, utakubaliana na hilo moja kwa moja ITUNE itaanza ku download software kwa ajili ya iphone yako. utasubiri mpaka imalize na  mwisho itafanya restore kwenye simu yako; MPAKA HAPO IPHONE yako itakuwa imerudi upya utaanza setting kama mwanzo.

kwa IPHONE X recovery mode
IPHONE x ina njia yake pekee ya kuifanya iwake kwa recovery mode ili uweze ku restore kwa hatua zilizoelezwa apo juu

Chomeka simu  IPHONE X kwenye computer yako kwa kutumia cable ile original iliyokuja nayo. zoezi linalofuata ni kibonya vitufe vya siphone x yako kwa mpangilio maalim ili kuifanya iwake kwa recovery mode.

utabonya kitufe cha kuongeza sauti kisha kwa haraka bonya cha kushusha sauti mwisho bonya halafu shilikia kitufe cha kulia usiachie mpaka simu itawaka kwenye mfumo wa recory mode.

Kama utakuwa na swali ama umekwama popote ama umefanikiwa  tuachie comment apo chini asante.

No comments:

Post a Comment