karibu text

KARIBU computerdevicedr

MAUJANJA BLOG

Uwanja wako pekee wa kupata maujanja mbali mbali kuhusu computer/device yako katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza kwenye matumizi ya computer/device yako. tuachie Maoni kwa jambo linalokutatiza Usaidike



Sunday 13 May 2018

KU INSTALL WINDOWS BILA KUPOTEZA DATA ZAKO

Changamoto hii tunaipata mara nyingi sana pale computer zetu zinapokuwa zime pata tatizo ambapo inalazimika ku install windows upya (kupiga chini) lakini unabaini kwamba kwnye computer yako kuna data muhimu ambazo hazitakiwi kupotea.

Leo tutapata maujanja njia mbili tofauti unazoweza kutumia katika kufanya installation bila kupoteza data zako muhimu kwenye computer.

NJIA YA KWANZA 
Ni kwa kutumia software ambozo zinaweza kuwasha computer yako kutoka kwekye flash ama cd bila ku install kwenye computer (live cd software) mfano. ububtu / Hiren's: Boot CD na nyinginezo.  
Hapa utawekamojawapo ya software izo kwenye flash yako ama uta andika kwenye cd yako na kisha uta washa mashine na kama kawaida kwa kutumia bios yako utafanya setting kwamba computer ianze kuwaka kutoka kwa flash ama cdrom yako kutegemea hiyo software yako umeweka wapi.
Kisha computer yako kuisoma ile software kwenye flash/ ama cd yako itawaka na kukupa muda wa kufanya backup ya data zako zote muhimu na baada ya apo ndipo uanze hatua ya ku install window yako.

NJIA YA PILI 
Hapa hakuna software yoyote ya pembeni utakayotumia, utatakiwa tu kuwa makini wakati wa istallation usiweze kupoteza data zako. utakachokifanya hapa ni kama kawaida utakuwa na cd yako ya windows ana kama ulishatengeneza flash yako ya window, utaweka kwenye computer yako na kufanya setting za bios kwamba computer ianze kuwaka toka kwa flash ama kwa cd yako ya window.
Kama kawaida computer ikishasoma cd ama flash yako itaweza kuwaka ikianza kukuletea hatua za installation kama kawaida.

Sasa hapa ndipo umakini unapotakiwa usiweze kupoteza data zako, utafuata muongozo kama ifuatavyo. haijalishi kama ulikuwa na window ya chini unataka ku install ya juu (mfano 7 na unataka 8 ama 10) ama unataka kurudisha window yako uliyokuwa nayo. - kwa wale walio na windowa 10 kuna njia nzuri zaidi ambayo haipotezi data inajulikana kama refresh.
(miongozo inafanana kwa windows zote apa utapata mfano kwa windows 7)
kama nilivyoeleza mwanzo ukiwa tayari umeshaandaa window cd ama flash yako na umesha fanya setting za bios kulingana kitu gani utatumia ku unstall window yako.
washa computer ukiwa umeshaweka cd ama kuchomeka flash
computer itasoma chanzo chako cha installation ka kukuletea miongozo ka ifuatavyo 


Hapa ndio installation inaanza utasubiri 
utachagua lugha alafu utabonya next 
apa utakubali terms  za Microsoft alafu bonya next 
apa utachagua option ya custom(advance) na sio upgrade 
sasa apa ndipo umakini zaidi unapoitajika utachagua partition ile ile ambayo ilikuwa na windows yako ya awali, bila kufanya format (narudia tena kwa msisistizo usifanye format) na ukibonya tu next upata jumbe kwamba partition uliochagua tayari ina window na itakuwa saved kwenye folder linaoitwa "old windows", kubaliana na hilo kisha endelea.
hapa utasubiri installation imalize kazi na mwisho kabisa baada ya kila kitu kukamilika utaweza kupata datazako zote zikiwa safi kwenye folder linalopatikana kwenye drive c: linaitwa old windows 
ukifungua old windows folder utakuta folders nyingine nenda kwenye users folder na tafuta jina ulilokua utatumia kwenye computer kabla ya kupata shida umo utakuta data zako zote salama salmin.

Mpaka hapo utakuwa umemaliza zoezi, kama una sawali ama unaitaji maelezo tuachie comment yako apo chini.

1 comment: