karibu text

KARIBU computerdevicedr

MAUJANJA BLOG

Uwanja wako pekee wa kupata maujanja mbali mbali kuhusu computer/device yako katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza kwenye matumizi ya computer/device yako. tuachie Maoni kwa jambo linalokutatiza Usaidike



Thursday 3 May 2018

COMPUTER KUPOTEZA KUMBUKUMBU

mara nyingi tumekutana na wadau wakilalamika ya kwamba computer zao zinapoteza settings ikiwemo majira kila mara zikiwaka na kusababisa mambo mengi yasiwe sawa kwenye computer husika.

ikiwemo kupata matakizo wakati una install baadhi ya software ama wakati unafungua internet kwa kutumia browser kama Mozilla na nyinginezo (kupata error ya certificate na vitu kama ivyo.
computer ikifikia hatua hii inatia hasira sana kwani itakulazimu ku set kila kitu upya kila ikiwaka, lakini si kwamba ndio mwisho wake umefika.. bado unaweza ukiweka sawa kwa  kubadilisha kitu kidogo sana chenye gharama ndogo kwenye motherboard yako (cmos battery). 
cmos battery (jina la madukani lithium battery) ni battery inayokaa kwenye motherboard ya computer yako na kazi yake kubwa ni kutunza kumbukumbu za setting zote za computer wakati wote ata kama computer imezimwa.
Hii battery inaweza kudumu kwa miaka kadhaa na kuna muda ukifika inaisha nguvu na kusababisha computer kupoteza kumbukumbu.
kutibu shida hiyo kwenye computer yako unatakiwa kufungua computer case yako na kuangalia kwa makini kwenye board yako na utaona battery na kama inavyoonekana pichani. utabonya kitufe cha kutolea battery kama tulivyokionyesha na utaweza kubadi na kuweka mpya. 
baada ya hapo utawasha computer yako na kufanya setting zako na computer yako itakuwa mpya tena.
ZINGATIA
Kwa laptops zinatofautiana wapi cmos battery inakaa na namna gani ya kuweza kubadili. ukiwa na shida ya laptop tuachie comment ikiwa na aina na model ya laptop yako tuweze kukupa maujanja. 
ukiwa na shaka jinsi ya kufanya zoezi usisite kutucheki kwenye contact page yetu tukusaidie ana kwa ana kwa ada nafuu kabisa sawa na bure

1 comment:

  1. Computerdevicedr Maujanja: Computer Kupoteza Kumbukumbu >>>>> Download Now

    >>>>> Download Full

    Computerdevicedr Maujanja: Computer Kupoteza Kumbukumbu >>>>> Download LINK

    >>>>> Download Now

    Computerdevicedr Maujanja: Computer Kupoteza Kumbukumbu >>>>> Download Full

    >>>>> Download LINK CB

    ReplyDelete