karibu text

KARIBU computerdevicedr

MAUJANJA BLOG

Uwanja wako pekee wa kupata maujanja mbali mbali kuhusu computer/device yako katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza kwenye matumizi ya computer/device yako. tuachie Maoni kwa jambo linalokutatiza Usaidike



Thursday 3 May 2018

JINSI YA KUONDOA AUTOMATIC UPDATES WINDOWS 10

kwa kweli hichi kitu kimekua kama ni janga kwa watu wachumi kama sisi. mpaka sasa imefikia hatua baadhi ya watu wanakutaka kuacha kutumia kabisa windows 10 na wengine wameshaacha kabisa kwa kisingizio kwamba inakula sana bundle. (kikubwa kinacho wachanganya zaidi ni kwamba windows 10 haina option za kuzuia updates kwenye control panel au setting apps kirahisi as  zilivyokuwa windows za nyuma.


kwa Jinsi ilivyo hakuna windows yoyote isiyokula bundle iwe xp 7 8 na at 10(maana ni lazima windows ifanye updates ili kwenda na wakati upande wa security na performance pia. 

kama sio mtumiaji wa internet mara kwa mara kwenye computer yako ni wazi kwamba operating system uliyonayo (windows)  kuwa itakuwa nyuma ukilinganisha na computer inayotumika kwenye internet mara kwa mara.
hivyo basi computer yako kwa kuwa ilikuwa haitumiki na internet kwa muda mrefu itakuwa na kiu ya updates kiasi kwamba  uki connect tu na internet itafanya updates kwa kiwango kikubwa mno kufidia updates zote ambazo haikuwahi kupata apo awali,  kiasi kwamba inaweza kukufanya uwe mkali kwa  provider wa mtandao unaotumia ukadhani wana hujumu  bundles zako.


ukweli ni kwamba updates ni ni muhimu sana kwa computer yako lakini inapobidi unaweza uka zuia sisifanyike hususan kama hukutumia internet mda mrefu kwenye computer na unataka kutumia internet kwa kazi yako ndogo ya mtandaoni, kama haujajiandaa kwa kuweka bundle ya kutosha unaweza kuzuia update zisifanyike mpaka utakapo kuwa vizuri ndipo uruhusu tena. 


Maujanja ya kuzuia kwa windows 10 isifanye updates 

hili linawezekana kwa ku  disable the Windows Update Service. kupitia  Control Panel > Administrative Tools

1. Right-click kwenye kitufe cha start  kufungua  WinX Menu. chagua  Run. Hii itafungua Run box. apo uta type  services.msc ndani yake kisha uta bonya  Enter kufungua  Services Manager.

service window ikifunguka shuka chini mpaka utakuta windows update apo uta left click alafu uchague properties 
Kwenye window itakayo funguka baada ya kibonya properties, utachagua  disable kisha OK kufunga updates 
mpaka hapo utakuwa umemaliza zoezi, kwa chochote Tafadhali tuachie comment apo chini..
n.b endapo utafanya process hii na bado ukaona computer yako inakula sana bundle kuliko kwaida unaweza ku kagua kama kuna software yoyote ya ku download inayofanya kazi kama hakuna ni dalili ya virus. 

1 comment: