karibu text

KARIBU computerdevicedr

MAUJANJA BLOG

Uwanja wako pekee wa kupata maujanja mbali mbali kuhusu computer/device yako katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza kwenye matumizi ya computer/device yako. tuachie Maoni kwa jambo linalokutatiza Usaidike



Wednesday 24 October 2018

LAPTOP KUZIMA MARA KWA MARA YENYEWE UKIWA UNAFANYA KAZI

watu wengi wameshapata changamoto hii na wasijue hasa nini kinachofanya hili litokee, na wakati mwingine kuishia kupeleka laptop kwa mafundi wasio waaminifu na kupigwa pesa wakipewa maelezo ya kwamba vifaa kadhaa hafifai (vimekufa).
leo utapata maujanja nini kifanyike kutatua changamoto hiyo bila kupasuka kichwa sama ana kutumia ghalama kubwa.
changamoto hii ya kuzima kwa laptop mara kwa mara yenyewe mara nyingi uletwa na vumbi zinazojaa kwenye fan ya ndani ya laptop inayopooza CPU na kufanya mashine kushindwa kupozwa vizuri na kupelekea changamoto hiyo ya kujizima mara kwa mara ukiwa unatumia.
dawa apa ni kusoma menu ya laptop husika na kuifungua hadi uikute ile FAN ambayo ndio inapooza processor  nayo pia utaifungua ndipo uisafishe na kuhakikisha vumbi lote limetoka.
Vumbi kwa kuwa limejikusanya kwa muda mrefu huwa linatengeneza kitu kama sponchi ambapo huziba kabisa vitundu vya kufanya hewa itoke na iingie vizuri na kupoza processor, hivyo kupelekea laptop kuzima kila ukiwasha na kutumia kwa muda mfupi tu (processor ina overheat).
Endapo umefanya solution hii na bado ya mashine haijakaa murua, apo waweza kutucheki kwa msaada Zaidi yawekana shida isiwe ni hiyo FAN peke yake.

2 comments: