karibu text

KARIBU computerdevicedr

MAUJANJA BLOG

Uwanja wako pekee wa kupata maujanja mbali mbali kuhusu computer/device yako katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza kwenye matumizi ya computer/device yako. tuachie Maoni kwa jambo linalokutatiza Usaidike



Thursday 17 May 2018

FAHAMU TEAMVIEWER NA VIPI INAWEZA KUOKOA SIKU YAKO

Wadau leo tutapata maujanja ya software moja ambayo inaweza kuokoa sana siku yako.


TeamViewer

Hii ni software ambayo inaweza kurahisisha sana maisha haswa kwa watu wa technical kwa kuwa software hii inaweza kufanya kitu kinaitwa (remote access) yaani uwezo wa ku control computer moja kwa kutumia computer nyingine ukiwa mbali nayo. (mfano kama uko na computer dar es salaam na wewe uko ata kama UK unachofanya una install software kwenye computer yako na kwenye computer upande wa pili pia software iwe installed.
pia software hii inafanya kazi kwenye vifaa vingine kama tablets na smart phones ivyo una uwezo wa ku access computer iliyo mbali ata kwa kutumia smartphone ana tablet yako. 

kwa watu wa technical mnaweza kusaidiana kitu kama mtu amekwama na wewe ndio expert ya kitu hicho, nyote mta fungua team viewer na utaweza ku access desktop ya Rafiki yako na kum assist safi kabisa kama vile uko eneo hilo
(mnaweza ku chatt kwa msg ama video na Rafiki unae mu assist live)

kwa watu wa kawaida unaweza kuwa  umesahau files zako muhimu kwenye computer yako na umesafili  bila computer na utaitaji izo file utaweza kuzipata, team viewer ndio njia pekee rahisi kwani ukitumia software hii kama kawaida utaweza ku access desktop yako ikiwa ni pamoja na kuperuzi computer yako kwa  kokote utakako na ku copy file lako muhimu ki lainiiii ata kwa kutumia tu tab au smartphone yako
(hakuna tena presha ya kuwa umesahau file muhimu maujanja ni team viewer)


cha kuzingatia wakati wa installation uchague option ya personal ili kutumua free  

cheki apa kupakua software hiyo
kwa kifaa smart device yako ingia kwa store yako na pakua bure kabisa

Wednesday 16 May 2018

KU RESTORE MAC YAKO KWA INTERNET IKIWA IMEKUFA AU UMEBADILI HDD MPYA

leo tutapata maujanja jinsi gani ya kurekebisha mac yako na kuirudisha kuwa safi (format) kwa internet. 
njia hii ni njia nzuri sana na salama zaidi ya ku restore mac yako, njia hii itapunguza hekaheka njingi unazoweza kupata ukitumia njia nyingine ku restore.
utatakiwa kuwa na internet enye kwenda vizuri bila ku kata kata (stable) na pia uwe na bundle sio chini ya 5gb 


JINSI YA KUANZA 
Utawasha mac yako na kwa kutumia keyboard yako utabonya key 3 kwa pamoja ukiwa unawasha mac yako (option command + ) 

ukiwa umebonya izo key 3 kwa pamoja moja kwa moja utapelekwa kwenye recovery mode 
utaendelea kufuata muongozo kutoka kwenye screen yako 
apa utachagua wireless yako na kuweka password zako kama zipo


hatua hii ndipo umakini unapotakiwa zaidi kwa kuwa unataka ku restore mac yako na kuwa fresh kabisa kama mpya, utatakiwa kwanza uende kwenye disk utility ili ku format kabisa ndipo urudi kwenye re install os x, ukianza na reinstall osx moja kwa moja utaweza kupata errs zitakazokupa changamoto 

Ndani ya disk utility utafuta data tayari kwa kuanza reinstallation ya os x 
baada ya apa utarudi nyuma na kuendelea na installation na mac os x kwenye mashine yako, fuatiza tu miongozo inayotoka kwenye kioo mpaka unapimaliza kufanya restore mac yako. 
mpaka hapo utakuwa ushamaliza ku restore mac yako na itakuwa safi kama mpya. enjoy
kama una swali tafathali comment apo chini 

Sunday 13 May 2018

KU INSTALL WINDOWS BILA KUPOTEZA DATA ZAKO

Changamoto hii tunaipata mara nyingi sana pale computer zetu zinapokuwa zime pata tatizo ambapo inalazimika ku install windows upya (kupiga chini) lakini unabaini kwamba kwnye computer yako kuna data muhimu ambazo hazitakiwi kupotea.

Leo tutapata maujanja njia mbili tofauti unazoweza kutumia katika kufanya installation bila kupoteza data zako muhimu kwenye computer.

NJIA YA KWANZA 
Ni kwa kutumia software ambozo zinaweza kuwasha computer yako kutoka kwekye flash ama cd bila ku install kwenye computer (live cd software) mfano. ububtu / Hiren's: Boot CD na nyinginezo.  
Hapa utawekamojawapo ya software izo kwenye flash yako ama uta andika kwenye cd yako na kisha uta washa mashine na kama kawaida kwa kutumia bios yako utafanya setting kwamba computer ianze kuwaka kutoka kwa flash ama cdrom yako kutegemea hiyo software yako umeweka wapi.
Kisha computer yako kuisoma ile software kwenye flash/ ama cd yako itawaka na kukupa muda wa kufanya backup ya data zako zote muhimu na baada ya apo ndipo uanze hatua ya ku install window yako.

NJIA YA PILI 
Hapa hakuna software yoyote ya pembeni utakayotumia, utatakiwa tu kuwa makini wakati wa istallation usiweze kupoteza data zako. utakachokifanya hapa ni kama kawaida utakuwa na cd yako ya windows ana kama ulishatengeneza flash yako ya window, utaweka kwenye computer yako na kufanya setting za bios kwamba computer ianze kuwaka toka kwa flash ama kwa cd yako ya window.
Kama kawaida computer ikishasoma cd ama flash yako itaweza kuwaka ikianza kukuletea hatua za installation kama kawaida.

Sasa hapa ndipo umakini unapotakiwa usiweze kupoteza data zako, utafuata muongozo kama ifuatavyo. haijalishi kama ulikuwa na window ya chini unataka ku install ya juu (mfano 7 na unataka 8 ama 10) ama unataka kurudisha window yako uliyokuwa nayo. - kwa wale walio na windowa 10 kuna njia nzuri zaidi ambayo haipotezi data inajulikana kama refresh.
(miongozo inafanana kwa windows zote apa utapata mfano kwa windows 7)
kama nilivyoeleza mwanzo ukiwa tayari umeshaandaa window cd ama flash yako na umesha fanya setting za bios kulingana kitu gani utatumia ku unstall window yako.
washa computer ukiwa umeshaweka cd ama kuchomeka flash
computer itasoma chanzo chako cha installation ka kukuletea miongozo ka ifuatavyo 


Hapa ndio installation inaanza utasubiri 
utachagua lugha alafu utabonya next 
apa utakubali terms  za Microsoft alafu bonya next 
apa utachagua option ya custom(advance) na sio upgrade 
sasa apa ndipo umakini zaidi unapoitajika utachagua partition ile ile ambayo ilikuwa na windows yako ya awali, bila kufanya format (narudia tena kwa msisistizo usifanye format) na ukibonya tu next upata jumbe kwamba partition uliochagua tayari ina window na itakuwa saved kwenye folder linaoitwa "old windows", kubaliana na hilo kisha endelea.
hapa utasubiri installation imalize kazi na mwisho kabisa baada ya kila kitu kukamilika utaweza kupata datazako zote zikiwa safi kwenye folder linalopatikana kwenye drive c: linaitwa old windows 
ukifungua old windows folder utakuta folders nyingine nenda kwenye users folder na tafuta jina ulilokua utatumia kwenye computer kabla ya kupata shida umo utakuta data zako zote salama salmin.

Mpaka hapo utakuwa umemaliza zoezi, kama una sawali ama unaitaji maelezo tuachie comment yako apo chini.

Wednesday 9 May 2018

NINI CHA KUFANYA UKIPATA ERROR WAKATI WA KU RESTORE/UPDATE IPHONE, IPAD AU iPOD

Tumekua kunapata error za aina mbali mbali wakati tukiwa tuna restore / update iphone, ipad, na apod zetu bila kubaini nini hasa kisababishi. 
leo tutapata dondoo kwamba nini cha kuangalia kwanza ukiwa unapata error wakati una update/restore iphoe,ipad,apod yako. 

MAMBO YA KUANGALIA 

1. utahakikisha utatumia itune version mpya kabisa (pata latest version hapa)  
2. hakikisha ume update operation system yako (windows/mac)

3. Tumia cable original na uchomeke moja kwa kwenye computer yako usitumie HUB ama connector ya aina yoyote.

4. Zima computer yako pamoja na device yako alafu washa tena
5. Angalia security software kwenye computer yako maana ziko software nyingine zinazoweza ku kinzana na connection kati ya computer itune na device ivyo unaweza kulazimika ku disable ama ku unistall security software husika kwanza. (security softwarezinazotengenezwa na kampuni nyingine tofauti na apple zinaweza kuzuia itune kuwasiliana na apple servers au devices)
6. jaribu tena ku restore/update device
kwa swali lolote Tafadhali comment apo chini 

Tuesday 8 May 2018

JINSI YA KU INSTALL NORTON SECURITY MPYA

Norton security ni latest computer software security suite iliyotolewa na wakongwe symentic. inafanya kazi na ms windows, mac os x, android, and ios platforms. zinapatikana kwa editions 3, norton security standard, norton security deluxe, na norton security premium.
norton security standard kwa 1 device, norton security deluxe kwa 5 devices, na norton security premium kwa mpaka 10 devices.
pia zinapatikana kwa (special editions)
NAMNA YA KUFANYA INSTALLATION 

unaweza ku install kwa online ama kutoka kwa cd uliyonunua kutoka kwa dealer (tucheki computerdevicedr 0767240679- tunazo kwa bei nafuu sana)
https://computerdevicedr.wixsite.com/tanzania/shop

tunaanzan na ku install kutoka kwenye cd moja kwa moja, utaweka cd ya norton security kwenye computer yako, na baada ya muda kidogo kawa kawaida ya installations tulivyozoea ita pop window ambayo ita ku guide kwenye installation nzima. 
Hatua ya mwishoni utapata muongozo wa ku log in na norton account kama huna utatakiwa kufungua norton account mpya. 


Apa utajiuliza kwa nini ufungue account?...... account ya norton security ina msaada mkubwa sana kwenye installation za norton security pale ambapo una install kwenye device zaidi ya moja. 
Pia itakusaidia endapo device yako imepata shida ukaitaji ufanye installation upya norton security ata kama umesahau/umepoteza KEY ukiwa na account ya norton security uki log in umemaliza kila kitu kinajiweka sawa.

Si ivyo tu pia ukuwa una install device zaidi ya moja na una KEY ya device zaidi ya moja pia uki log in tu kwa norton security kutumia na accounti yako wakati una install device nyingine kila kitu kinakuwa activated automatically.

Nilichopenda zaidi ni kwamba mfano kama ume install kwenye computer yako  ya home na umesafiri ghafla na laptop yako na hautaki ku risk lakini hujapata mda wa kununua norton security fasta fasta kwenye laptop, unaweza uka download kutoka  internet alafu uka log in kwa ile account ya computer yako ya home na fasta utapewa option kama unataka kuamisha license na ukikubali laptop inakuwa full activated kutumia licence ya kwenye computer ya home na Maisha yanaenda saaaafiii😎😎😎😎😋….. norton aisee chiboko kweli mkongwe mkongwe tu.

kwa installation ya  kwenye mobile device utaingia kwenye app store yako na ku download norton security   kisha install na utamaliza kwa kuweka key ambayo umepata wakati wa kunua. 
mpaka apo. utakuwa umeshamaliza installation yako. kama hko na sawali acha comment yako apo chini.

Sunday 6 May 2018

MAUJANJA 8TOKA KWA KEYBOARD YAKO YATAKAYO RAHISISHA MAISHA

Tumekua na mazoea ya kutumia keyboard na mouse katika kazi zetu nyingi tunatozifanya kwenye computer zetu. kuna baadhi ya program bado zinaweza kukupa changamoto kufanya kazi yako kwa haraka zaidi kama hutofamu maujanja ya utumiaji wa keyboard yako kukurahisishia Maisha. 

Leo tutawaletea maujanja 8toka kwa keyboard yako ambayo bila kuwa nayo unaweza kujikuta unakwama ama unachukua muda mrefu sana kufanya jambo moja dogo kwenye baadhi ya program 

maujanja 
1ctrl + a= hutumiaka kuchagua kilakitu, yaweza kuwa ni maandishi ana ata ma file au ma folder 
(cmd + a) kwa computer za apple 

2. ctrl + c = hutumika ku copy taalifa unazotaka baada ya kuwa umesha zichagua
(cmd + c) kwa computer za apple

3. ctrl +v = hutumika ku paste taarifa zako
(cmd +v ) kwa computer za apple 

4. PC : Ctrl + Z au Ctrl + Y = hutumika kwa ku undo ama ku redo changes. ambapo Ctrl + z = undo na Ctrl + y = redo 
kwa computer za Apple: Cmd + Z au Cmd + Y

5. PC: Ctrl + Home or Ctrl + End = hutumika kuhamisha cursor mwanzo ama mwishoni kwa document, ambapo Ctrl + Home = mwanzo wa document na Ctrl + End mwiho wa document 
kwa computer za apple : Cmd + up arrow or Cmd + down arrow

6. PC Shortcut: Ctrl + S and Ctrl +P = Hutumika kwa ku save ama ku print, ambapo Ctrl +S = Save na Ctrl + p = print 
Apple computers: Cmd + S and Cmd + P

Windows computers: Ctrl + F = hudumika kwa kutafuta neon kwa document au ata file ama folder 
kwa computer za Apple  : Cmd + F

8 Watumiaji wa apple computers waweza kufungua tab mpya kwenye google crome kirahisi kwa Cmd + t na kufunga tab kwa  Cmd + w.

hayo ni maujanja 8 yanayoweza kufanya siku yako ikawa nyepesi kabisa.. kama una swali ama una maujanja mwngine makali unaweza ukaacha comments apo chini 

Friday 4 May 2018

FAHAM TOFAUTI YA HDD NA SDD


          HDD                 SDD



HDD - HARD DISK DRIVE
SSD - SOLID STATE DRIVE 
Hizi zote mbili zinafanana katika nini kazi yake kwenye computer zetu, zote kazi yake ni kuifadhi taalifa tunazo save kwenye computers.
Utofauti hapa ni technology tu kama tulivyozoea toka awali HDD - hard disk drives ndizo technology ya kwanza katika nyanja hii ya storage. 
Kama tunavyofahamu HDD zimeundwa kuifadhi data kutumia mechanical (moving parts)  read / write head, na spinning plate lakini tofauti na SSD hizi hazijaundwa kwa mfumo huo zenyewe huifadhi data kwa mtindo wa wa microchips kama vile flash drives.
kwenye SDD kwa kuwa hakuma moving parts ni microchips, hivyo hapa inaongeza hufanisi zaidi hususani katika swala zima la kusoma ama kuandika data.
Hivyo ndio kusema kwamba ukiwa na SSD kwenye computer yako ama laptop utabaini kwamba computer inawaka kwa haraka zaidi na unafungua program kwa haraka zaidi kuliko HDD
Kwa sasa SSD Technology inaonekana kushika kasi zaid maana kwenye computer zilizopo sokoni sasa ivi zinakuja na SSD hususan laptop, ingawa bado hazijaanza kutoka kwa size kubwa kubwa kama tulivyozoea kwenye HDD. 
Tofauti nyingine ni upande wa bei, ambapo DRIVE zinazotumia SSD technology zinakuwa na bei kubwa zaidi kuliko HDD wakati mwingine ata kama HDD ni kubwa kwa size.
ni hayo tu kwa uchache kuhusu HDD na SDD. kama una swali unataka kujua zaidi tuachie comment apo chini 

Thursday 3 May 2018

JINSI YA KUONDOA AUTOMATIC UPDATES WINDOWS 10

kwa kweli hichi kitu kimekua kama ni janga kwa watu wachumi kama sisi. mpaka sasa imefikia hatua baadhi ya watu wanakutaka kuacha kutumia kabisa windows 10 na wengine wameshaacha kabisa kwa kisingizio kwamba inakula sana bundle. (kikubwa kinacho wachanganya zaidi ni kwamba windows 10 haina option za kuzuia updates kwenye control panel au setting apps kirahisi as  zilivyokuwa windows za nyuma.


kwa Jinsi ilivyo hakuna windows yoyote isiyokula bundle iwe xp 7 8 na at 10(maana ni lazima windows ifanye updates ili kwenda na wakati upande wa security na performance pia. 

kama sio mtumiaji wa internet mara kwa mara kwenye computer yako ni wazi kwamba operating system uliyonayo (windows)  kuwa itakuwa nyuma ukilinganisha na computer inayotumika kwenye internet mara kwa mara.
hivyo basi computer yako kwa kuwa ilikuwa haitumiki na internet kwa muda mrefu itakuwa na kiu ya updates kiasi kwamba  uki connect tu na internet itafanya updates kwa kiwango kikubwa mno kufidia updates zote ambazo haikuwahi kupata apo awali,  kiasi kwamba inaweza kukufanya uwe mkali kwa  provider wa mtandao unaotumia ukadhani wana hujumu  bundles zako.


ukweli ni kwamba updates ni ni muhimu sana kwa computer yako lakini inapobidi unaweza uka zuia sisifanyike hususan kama hukutumia internet mda mrefu kwenye computer na unataka kutumia internet kwa kazi yako ndogo ya mtandaoni, kama haujajiandaa kwa kuweka bundle ya kutosha unaweza kuzuia update zisifanyike mpaka utakapo kuwa vizuri ndipo uruhusu tena. 


Maujanja ya kuzuia kwa windows 10 isifanye updates 

hili linawezekana kwa ku  disable the Windows Update Service. kupitia  Control Panel > Administrative Tools

1. Right-click kwenye kitufe cha start  kufungua  WinX Menu. chagua  Run. Hii itafungua Run box. apo uta type  services.msc ndani yake kisha uta bonya  Enter kufungua  Services Manager.

service window ikifunguka shuka chini mpaka utakuta windows update apo uta left click alafu uchague properties 
Kwenye window itakayo funguka baada ya kibonya properties, utachagua  disable kisha OK kufunga updates 
mpaka hapo utakuwa umemaliza zoezi, kwa chochote Tafadhali tuachie comment apo chini..
n.b endapo utafanya process hii na bado ukaona computer yako inakula sana bundle kuliko kwaida unaweza ku kagua kama kuna software yoyote ya ku download inayofanya kazi kama hakuna ni dalili ya virus. 

COMPUTER KUPOTEZA KUMBUKUMBU

mara nyingi tumekutana na wadau wakilalamika ya kwamba computer zao zinapoteza settings ikiwemo majira kila mara zikiwaka na kusababisa mambo mengi yasiwe sawa kwenye computer husika.

ikiwemo kupata matakizo wakati una install baadhi ya software ama wakati unafungua internet kwa kutumia browser kama Mozilla na nyinginezo (kupata error ya certificate na vitu kama ivyo.
computer ikifikia hatua hii inatia hasira sana kwani itakulazimu ku set kila kitu upya kila ikiwaka, lakini si kwamba ndio mwisho wake umefika.. bado unaweza ukiweka sawa kwa  kubadilisha kitu kidogo sana chenye gharama ndogo kwenye motherboard yako (cmos battery). 
cmos battery (jina la madukani lithium battery) ni battery inayokaa kwenye motherboard ya computer yako na kazi yake kubwa ni kutunza kumbukumbu za setting zote za computer wakati wote ata kama computer imezimwa.
Hii battery inaweza kudumu kwa miaka kadhaa na kuna muda ukifika inaisha nguvu na kusababisha computer kupoteza kumbukumbu.
kutibu shida hiyo kwenye computer yako unatakiwa kufungua computer case yako na kuangalia kwa makini kwenye board yako na utaona battery na kama inavyoonekana pichani. utabonya kitufe cha kutolea battery kama tulivyokionyesha na utaweza kubadi na kuweka mpya. 
baada ya hapo utawasha computer yako na kufanya setting zako na computer yako itakuwa mpya tena.
ZINGATIA
Kwa laptops zinatofautiana wapi cmos battery inakaa na namna gani ya kuweza kubadili. ukiwa na shida ya laptop tuachie comment ikiwa na aina na model ya laptop yako tuweze kukupa maujanja. 
ukiwa na shaka jinsi ya kufanya zoezi usisite kutucheki kwenye contact page yetu tukusaidie ana kwa ana kwa ada nafuu kabisa sawa na bure

Wednesday 2 May 2018

NINI CHA KUFANYA KWA DISABLED IPHONE

Kutokana na maombi ya mdau mmoja wa computerdevicedr maujanja blog, leo naweletea maujanja nini cha kufanya endepo iphone yako imekua disabled.
ujumbe wenye muonekano wa namna hii kwenye iphone yako waweza kukupa sononeko kubwa mno na ukijue nini cha kufanya. chanzo cha jumbe kama hiyo kwenye iphone ni kuwa mtumiaji anakuwa amesahau password yaka ma kujaribu mara nyingi mpaka kupelekea simu kuwa disabled 
kwa hali ya kawaida apa tungesema picha limeisha maandishi matatu the end, lakini kutoka maujanja blog leo utafahamu ni namna gani utachomoka kwenye sononeko hili na kuokoa fuba ambalo ungekiacha kwa wataalaam.

Hatua za kufanya / maandalizi 
awali ya yote hakikisha una kumbuka vizuri apple ID yako. 
1. hakikisha una computer ya windows ama MAC
2. uwe umesha install ITUNE version mpya kabisa
3. uwe na internet stable (isiwe inakata kata)
4. uwe na bundle ya kutosha kuanzia 5gb ukiweza ata 10gb kwa uhakika

kitakacho fuata hapa baada ya kuhakiki vitu vyote viko sawa ni kuchomeka simu yako kwenye computer (lakini kwa mtindo wa recovery mode)
- kuifanya iphone yako recovery mode kuanzia iphone za mwanzo ama zile zote zenye (home button) uta chomeka cable kwenye simu yako alafu huku umeshika home button bila kuachia chomeka cable kwenye computer. hapo simu yako itaonekana kwenye kioo ikiwa na alama ya itune ikiashiria tayari iko recovery mode.
(Alama hii ya ITUNE inaweza kuwa tofauti kwa rangi hilo lisikuogopeshe bado upo sawa hiyo ni kutokana na model ama software ulionayo kwa iphone yako.)

mambo yote ya kiwa sawa upande wa computer yako program ya ITUME itaisoma simu na kutoa taarifa kwamba utaitaji kuifanyia restore/update, utakubaliana na hilo moja kwa moja ITUNE itaanza ku download software kwa ajili ya iphone yako. utasubiri mpaka imalize na  mwisho itafanya restore kwenye simu yako; MPAKA HAPO IPHONE yako itakuwa imerudi upya utaanza setting kama mwanzo.

kwa IPHONE X recovery mode
IPHONE x ina njia yake pekee ya kuifanya iwake kwa recovery mode ili uweze ku restore kwa hatua zilizoelezwa apo juu

Chomeka simu  IPHONE X kwenye computer yako kwa kutumia cable ile original iliyokuja nayo. zoezi linalofuata ni kibonya vitufe vya siphone x yako kwa mpangilio maalim ili kuifanya iwake kwa recovery mode.

utabonya kitufe cha kuongeza sauti kisha kwa haraka bonya cha kushusha sauti mwisho bonya halafu shilikia kitufe cha kulia usiachie mpaka simu itawaka kwenye mfumo wa recory mode.

Kama utakuwa na swali ama umekwama popote ama umefanikiwa  tuachie comment apo chini asante.

Tuesday 1 May 2018

NINI CHA KUFANYA UKIWA UMESAHAU PASSWORD YA SIMU YA ADROID

Changamoto nyingine ambayo watu wengi wanakutana nayo haswa wale wanaokua na mabo mengi ni usahaulifu wa password am walizoweka kwenye simu zao.
apa utapata maujanja ni kwa namna gani unaweza kuchomoka kwenye janga hili na ukawa umeokoa siku yako.
njia ya kwanza:- hii inafanya kazi kama unatumia adroid version za nyuma kidogo kama hujui unatumia adroid gani unaweza kujaribu njia hii kwanza kwa kua ni nyepesi zaidi. apa utakachofanya ni kujaribu kuweka password ambayo sio sahihi mara nyingi na mwishoni utapata jumbe inayokuelekeza kuwa umejaribu kuweka password mara nyingi na ufungue kwa email address 
kwa kuwa utakuwa unakumbuka email na password yako ya gmail ukiweka api simu yako itafanikiwa kufunguka na utaendelea ku enjoy kama kawa 

njia ya pili:- hii inatumika kwa wale wanaotumia adroid version mpya mpya na kama maujanja ya kwanza hayajafanya kazi basi hii itamaliza shida. zingatia kwamba njia hii itafuta data zote kwenye simu yako na itakuwa kama simu mpya.
utabonya vitufe vitatu kwa mara moja kwenye simu yako ukiwa inaiwasha  yaani kitufe cha kuongeza sauti na cha (kuzima / kuwasha) pamoja na home

kila kitu kikienda sawa simu itakupeleka kwenye recovery mode apo utakuwa unachagua sehehu inayosema (wipe data factory reset) utatumia kitufe cha kuongeza / kupunguza sauti katika kupanda ama kushuka na kitufe cha kuzimia/kuwashia simu kwa kuchagulia chaguzi
kwa kufanya hilo zoezi utakuwa uweshafuta simu yote na utaanza upya na settings kama ilivyokua mpya. 

kwa apo utakuwa umefnikiwa pia ku rekebisha simu yako. ukiweka password mpya hakikisha una hifadhi maala kuepuka kupoteza taarifa zako muhimu mara kwa mara.
kama unaswali ama haujaelewa mahali vizuri acha commet yako hapa chini