karibu text

KARIBU computerdevicedr

MAUJANJA BLOG

Uwanja wako pekee wa kupata maujanja mbali mbali kuhusu computer/device yako katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza kwenye matumizi ya computer/device yako. tuachie Maoni kwa jambo linalokutatiza Usaidike



Sunday 27 October 2019

keyboard replacement lenovo t540p

Ni wakati mwingine wa kupata maujanja toka kwetu bure kabisa, leo ntawapa maujanja jinsi ya kubadilisha keyboard ya laptop yako aina ya Lenovo t540p (keyboard replacement )

cha kwanza kabisa unatakiwa kuwa na screwdriver ya flat na star kila moja itasaidia eneo lake katika kukamisha zoezi zima.

Hatua ya kwanza : kwa kutumia flat screwdriver pachua lock mbele kigogo ya keyboard kama inavyoonekana kwenye picha

Sasa utaweza kuoma screws zilizofuchwa katikati

Hatua ya pili : kwa kutumia screwdriver yako ya star fungua screws izo moja baada ya nyingine kama zinavyoonekana kwa mchoro
baaya ya kumaliza kufungua screws zote sasa slide keybord kwa nyuma kuitoa, kuwa makini kwa kua kuna mikanda inayojishika chini kwenye board usije ukakata.

Nyanya terminal zilizoshika kila mkanda kwenda kwa juu (kama inayoonekana mfano no.5) kisha ndio uchomoe kwa kuvuta kwa nyuma (kama inavyoonekana mfano no: 8 ) kuwa umakini na usitumie nguvu kuichomoa mikanda  (ukishanyanyua terminals mikanda inachokoka kiulaini kabisa
(mpaka hapo utakuwa umemaliza kutoa keyboard kwenye laptop yako)

Sasaa hatua zinazofuata ni za kurudishia keyboard kwenye laptop yako, ni rahisi kwa kuwa unakuwa unarudia hatua hizi kuanzia ya mwisho kwenda ya kwanza.

Utaanza na kuchomeka mkanda mmoja mmoja kisha unabana terminal zake kwenda chini kama inavyoonyeshwa mchoroni apo chini

kisha utapachika keyboard yako kuanzia upande wa mbele


sogeza tena keyboard kwa kutumia flat screwdriver kwa mbele kidogo ili upate kuona screw zilizofichika (mfano no: 7 pichani apa chini)

Funga screw moja moja mpaka umalize zote
Kwa kutumia flat screwdriver rudishia cover ya juu kwa nyuma kufunika screw ziaionekane (mfano no9 kwenye mchoro apo chini.



Mpaka apo utakuwa umemaliza zoezi la kutoa na kurudishia keyboard kwenye mashine ya Lenovo t540p. maujanja haya yanaweza kutumika pia kwenye model za Lenovo zinazofanana ha hii.







Thursday 30 May 2019

norton security free activation keys (first 5 users)


offer toka computerdevivedr: keys za kitonga kwa mwaka mzima bureee

1. JBPHFBKWG4TQR27G8B6693GYK
2. JD3B46VTG8CPBQK23V9DHXFCF
3. JPJGVXFMD9Q4BT27P3DXVYXWH
4. JCKW2GJFG868G4YFRWG924B8F
5. J438J2RK78BRCW8WVGK4XPTPB
kama mambo yako poa au unaitaji msaada jinsi ya ku activate tafadhali comment apo chini

Tuesday 26 February 2019

Huawei Mate X 5G Foldable Phone

Baada ya baadhi ya makampuni makubwa ya simu ikiwemo Samsung  kuonyesha simu za kisasa za kukunja ambazo zinaonyesha kuleta mapindizi makubwa kwenye uwanja wa smartphones.
nayo kampuni ya huwawei haijabaki nyuma kwa kuwa nayo ivi karibuni imeamua kuonyesha simu ya kukunja ambayo pia ni ya kwanza kuwa na 5g toka kampuni hiyo. (Huawei Mate x 5G)
Huawei Mate X ni nyembaba hatari  ni 5.4mm, 6.6 inch  19.5:9 OLED display ikiwa na   2480 x 1148 pixels resolution wakati ikiwa imekunjwa , 6.38 inch OLED 25:9 display ikiwa na  2480 x 892 pixels resolution kwa  panel ya njyuma na 8 inch OLED 8:7.1 display ikiwa na  2480 x 2200 pixels resolution wakati ikiwa imekunjuliwa .


kwa maelezo rahisi ,  device winakuja na  6.6 inch OLED screen on the front pamoja na 6.38 inch screen upande wa nyuma ikiwa imekunjuka, imbayo inafanya 8 inch display ikiwa imekunjuka . Huawei imetumia Falcon Wing designpamoja na  stretchable hinge ambayo iinapelekea device kuwa flat na smooth pande zote.

pata video uione kidogo video toka :(The Tech Chap)             


Sunday 27 January 2019

MICROSOFT WATASITISHA KU SUPPORT WINDOWS 7

kwa wale watumiaji wa windows 7 sasa ni wakati muafaka wa kufanya upgrade kwa kuwa Microsoft wametangaza rasmi kuwa kuanzia mwakani jan 14, 2020 hawata support windows 7, hii inamaanisha hakutakuwa na security updates fixes kwa operating system hii. (windows 7)
Ni wakati muafaka sasa kuweza kuama ama kuamisha kampuni yako toka kwenye windows 7 kwenda windows 10.
"mabadiliko kwenye technology hayaepukiki" alisema hayo Brad Anderson corporate vice president for Microsoft 365, kwenye blog 
Microsoft wataendelea ku support windows 7 kwa business users ambao wanalipia na sio kwa individual ussers.
windows 7 ilitoka tangu mwaka 2009 lakini bado ni operating system  inayotumika zaidi kwenye desktop/laptop za watu binafsi na hata kwenye makampuni  hadi sasa.
kwa kuanzia kufanya upgrade ya windows 7 kenda windows 10 tembelea apa kisha bonya download chini kidogo ya (Create Windows 10 installation media).
Apa utaweza ku download tool ambayo itakuwezesha kufanya upgrade ya windows yako. run iyo tool kisha chagua upgrade this pc option kisha fuata maelezo.

Thursday 8 November 2018

SAMSUNG HATIMAYE WAONESHA SIMU YAO YA KWANZA YA KU KUKUNJA (GALAXY X)

Baada ya tetesi za muda mrefu hatimae Samsung yaamua kuonyesha simu yao ya kukunja ya kwanza kabisa kwenye matoleo yake ya simu.
simu hii itakuwa na uwezo wa kukunjwa kuwa kama simu ya kawaida na pia ukiikunjua inakua as tablet.
Mambo haya ya kimaajabu yamewezekana kwa kua Samsung itatumia technologia yake mpya ya vioo  (infinity flex Display).  
Pia inasemekana kwa kutumia technology hii ya infinity flex display kwenye simu utaweza kufunga na kufungua simu mara nyingi upendavyo bila madhala yoyote. 

mcheki mzee mzima Justin Dension, Samsung senior vice president (mobile marketing) ameionyesha simu hiyo kwa mara ya kwanza huku ikiwa imefichwa kwenye cover jeusi, na kufanya ule muonekano halisi kwa maana ya umbo lake bado halijaonekana.  
Sambamba na haya kuna maboresho mengi mno Samsung inaendelea kufanya kwenye device zake zinazo kuja, endelea kutufuatilia kwa mengi zaidi. 

Saturday 27 October 2018

WHATSAPP KULETA HUDUMA YA STICKERS IVI KARIBUNI

WhatsApp imetangaza ivi karibuni itaongeza huduma ya stickers ambayo tayari ipo kwenye chatt apps nyingine kama vile bbm
huduma imeshaanza kuwafikia baadhi ya watumiaji wa ios na kwa kwatumiaji wa adroid bado ni beta version lakini ivi karibuni mambo yatakua mswano.
Sticker packs inakuja na  stickers kama  (smiling teacup, crying broken heart) na  zaidi, zilizoundwa na madesigner toka   WhatsApp na ma artists wengine pia.

Ukisha updated WhatsApp, utaona stickers icon baada tu ya emoji and GIF icons kwenye emoji menu. utapata tabs tau kama kawaida —moja ni ya  recent stickers, ya pili  ni ya favourites na ya tatu inabeba  stickers zote. pia kuna  “plus” icon kwenye kona ambayo itakuruhusu wewe ku add  stickers Zaidi kwenye  WhatsApp kupitia  sticker store.

kama hujazipenda stickers zilizokuja moja kwa moja na WhatsApp, unaweza tengeneza wewe mwenyewe. WhatsApp wametoa maelekezo namna gani utafanya —unaweza kusoma hapa lakini hili litaitaji ujuzi kidogo wa Adobe Photoshop na basic image editing. stickers zinaitaji kuwa na  resolution ya   512x512 pixels na zinatakiwa kuwa na file size ya chini ya 100kb.

Friday 26 October 2018

UNLOCK LAPTOP YAKO KUTUMIA FINGERPRINT YA SIMU - ANDROID




leo kwa haraka haraka tutapata maujanja apa, kuna wakati mtu unaweza ukawa kwenye public ha hupendi password yako ya laptop ionekane na wanazengo wengine.
sasa dawa ipo kwani unaweza ku fanya setting na kuwa unatoa lock ya laptop yako kutumia fingerprint ya simu yako.
Najua bado unajiuliza ni vipi mambo haya yanawezekana; maujanja kama haya utayapata apa computerdevicedr pekee.
Bila kupoteza muda vifuatavyo vitatakiwa kufanikisha
1. software kwa ajili ya computer _ link
2. software kwa ajili ya adroid yako _ link

software hii ina inafanya kazi kwenye mazingira yafuatayo;
  • x86 or x64
  • Windows Vista, Windows 7, Windows 8, or Windows 10 PCs
  • Android 6.0+

Software ni bure lakini ina option nyingine za kulipia ukipenda kama ifutavyo;

huduma za bure
  • Support for remotely unlocking both local and online Microsoft accounts via fingerprint    scanner
  • Utaseup PC 1 TU account 1 kufanya remote unlocking
  • Wi-Fi Tethering support
Huduma za kulipia (malipo $1.99)
  • No advertisements
  • kuongeza  computer Zaidi ya moja
  • kuongeza  account zaidi kwa pc 
  • ina support  kuamka -kenye-LAN
Namna gani ya ku setup
  • Download na install Remote Fingerprint Unlock from the Google Play Store.
  • Download na install the right Windows Fingerprint Credential Module kwa ajili ya Windows PC.
  • fungua   Android app nenda kwa  Scan section.
  • Anza Scan operation na acha app itafute PC yako.
  • bonya  kwenye   PC unayotaka ku set. unaweza kuchagua kuipa jina au tuma command ya Wake-on-LAN packet kama una huduma ya kulipia.
  • After adding the PC, go to the Accounts section.
  • bonya on “Add Account.” weka username and password ya account unayotaka kufanya remotely unlock.
  • baada ya ku add account , bonya kwenye jina la account iwe  (Selected) message saying something like “no default account has been selecte
  • sasa ,jaribu ku unlock pc yako .na utaona user mpya anaitwa “Fingerprint Unlock.” (bonya kama itasema If it says the module is active, apo uko vizuri
  • fungua  Remote Fingerprint Unlock na nenda kwenye unlock sectioction
  • Scan  fingerprint.
  • kama uliset vyema , utaona windows ina funguka safi, enjoy technology bwana kama uchawi vile ….

Wednesday 24 October 2018

LAPTOP KUZIMA MARA KWA MARA YENYEWE UKIWA UNAFANYA KAZI

watu wengi wameshapata changamoto hii na wasijue hasa nini kinachofanya hili litokee, na wakati mwingine kuishia kupeleka laptop kwa mafundi wasio waaminifu na kupigwa pesa wakipewa maelezo ya kwamba vifaa kadhaa hafifai (vimekufa).
leo utapata maujanja nini kifanyike kutatua changamoto hiyo bila kupasuka kichwa sama ana kutumia ghalama kubwa.
changamoto hii ya kuzima kwa laptop mara kwa mara yenyewe mara nyingi uletwa na vumbi zinazojaa kwenye fan ya ndani ya laptop inayopooza CPU na kufanya mashine kushindwa kupozwa vizuri na kupelekea changamoto hiyo ya kujizima mara kwa mara ukiwa unatumia.
dawa apa ni kusoma menu ya laptop husika na kuifungua hadi uikute ile FAN ambayo ndio inapooza processor  nayo pia utaifungua ndipo uisafishe na kuhakikisha vumbi lote limetoka.
Vumbi kwa kuwa limejikusanya kwa muda mrefu huwa linatengeneza kitu kama sponchi ambapo huziba kabisa vitundu vya kufanya hewa itoke na iingie vizuri na kupoza processor, hivyo kupelekea laptop kuzima kila ukiwasha na kutumia kwa muda mfupi tu (processor ina overheat).
Endapo umefanya solution hii na bado ya mashine haijakaa murua, apo waweza kutucheki kwa msaada Zaidi yawekana shida isiwe ni hiyo FAN peke yake.

Friday 21 September 2018

INSTALL ADROID 8 (OREO) AU ADROID 9 (PIE) KWA DEVICE YAKO YA ZAMANI

Kwa wale ambao bado wanatumia adroid devices za zamani kuanzia device za mwaka 2014 kushuka chini katika hali ya kawaida device izo zimekuwa zikibaki nyuma kwa kutumia android za version ya nyuma.
hivyo kufanya watumiaji wa device izo wengi kushindwa ku enjoy features mpya zinazokuja kila wakati toka kwa adroid versions mpya.
Wapo wanaoamua kuuza device zao ata kama bado wanazipenda na kulazimika kununua device mpya yote kwa sababu tu waweze kupata mambo mazuri toka kwenye adroid versions mpya. (mfano kwa sasa kuna adroid 8 oreo na Adroid 9 pie) ambapo device nyingi za zamani bado zimenasa kwenye adroid 6 marshmallow na chache zimejikongoja mpaka Android 7 Nougat.





Android zote mpya zimekuja na features nyingi mpya na kali zaidi kuliko kwenye adroid zilizopita.
Pamoja na features nyingi mpya pia zinafanya device yako kuwa na perfomance bomba zaidi bila kuliko mwanzo 

Leo tutapata kufaham namna gani tunaweza kupandisha android kwenye device zetu za zamani mpaka android 8 au 9

Tools za kuwa nazo ili kufanikisha
1. Custom recovery - link 
2. Lineage OS - link 
3. Google Apps - link
GAPPS zinazopendekezwa - link

kabla hujaanza chochote hakikisha device yako ina battery ya lutosha walau 60% kuepuka ku haribu kabisa 

Hatua
1. Download tools zote 3
2. Hakikisha unafanya backup ya device yako kwanza
2. Hatua inayofuata ni ku flash custom recovery
3. Kisha copy lineage OS na GApps kwenye device yako
4. Zima device yako kisha ipeleke kwa recovery mode. 
5. Anza kwa ku wipe factory
6. mwisho anza ku flash file moja moja kuanzia na lineage os kisha gapps

Baada ya kumaliza ku flash file zote mbili kama nilivyo eleza apo juu ukianza na lineage na kumaliza na gapps, uta re start device yako.
Muwako wa kwanza unaweza kuchukua muda kidogo so usipanic relax mpaka upate setup menu.
mpaka hapo mambo yatakua fureshi enjoyyy
kama una swali hujaelewa kufanya jambo lolote kati ya mambo tajwa apo juu, au umefanya jambo na umekwama maala usisite tuachie comment apo chihi…

Saturday 15 September 2018

TIGO YAZINDUA 4G+

kingine cha kwanza bomba toka Tigo.
Mara kwa mara kampuni ya simu za mkononi tigo imekuwa mstari wa mbele katika kuwapa walaji wake Huduma bomba zaidi.
kwa mara nyingine tena kampuni hii inakuwa ya kwanza Tanzania kuanzisha  Huduma ya 4G+ Huduma ya internet itakayonfanya Mteja wa tigo ku enjoy mtandao wa internet kwa speed kasi mara mbili zaidi kuliko ilivyo kwa 4G ya kawaida 
  
4G+ inakimbiza hadi 120 mbps ivyo kufanya Wateja wa Tigo sasa kufanya mambo mengi zaidi na kwa haraka zaidi mtandaoni.
Pamoja na kupata mwendo kasi mkubwa zaidi kuliko mitandao mingine Wateja wa tigo watalipa ghalama zile zile nafuu kabisa toka tigo.

Ili Mteja aweze ku faidi Huduma hii ya 4G+ anatakiwa tu kuwa na device inayo support Huduma hii na kuwa katika eneo linalotoa speed ya 4G+

ili kubaini kama device yako ina support hudumaa hii kwanza angalia imei yako kwa kubonya *#06#
kisha ingiza tarakimu nane za mwanzo hapa
kama device yako hai support Huduma hii usikonde cheki hapa ujionee device bomba utakazo zipata maduka ya tigo kwa bei bomba sana.

ukiwa na swali acha cooment yako apo chini kama kawa tutasema nayo.

Waweza piga 0658000097 tuchonge.

Tuesday 24 July 2018

JINSI YA KUFANYA PES KONAMI IONEKANE BOMBA



Kwa wale wapenzi wa games za computer, napozungumzia PES KONAMI nafikili watakuwa wananipata vizuri sana. 
kwa kifupi tu hii ni moja ya computer -football game inayofanya vizuri sana ukiachilia FIFA. zipo sababu mbali mbali zinazofanya baadhi ya wapenzi wa games hizi kuona kila moja ni zaidi ya nyingine.
sababu mojawapo ni kwamba FIFA inakuja ikiwa na full licence ambapo unapocheza unakuta imetimia kila kitu, kama vile team kuwa na jezi sahihi na logo za team kuwa ziko vizuri pia.
kwa upande wa PES yenyewe imebeba umaarufu kwa kuwa na graphics bomba na gameplay bomba pia.
Leo utapata maujanja vipi utafanya PES game yako iwe bomba zaidi wa kuifanya iwe na licence full kama ilivyo FIFA na kuifurahia zaidi kuicheza.
Maujanja apa ni kufanya pach ambayo itabadili kabisa muonekano wa PES game yako muwa bomba zaidi, wako developers wengi waliotoa patch mbali mbali za namna hii, lakini leo nakuletea developer maalufu sana kwenye njanya hizi, anakuja na pach ijulikanayo kama SMOKE PATCH 
https://www.pessmokepatch.com/
PATCH hii kwa kweli iko bomba mno kuliko patch nyingine nilizowahi kuzipitia developer yuko makini mno amegusa kila kitu kwenye game.

Friday 20 July 2018

TIGO JIHUDUMIE

umeshawahi kukosea kutuma pesa na bado ukawa UNATABASAMU?

(HAYO SASA YANAWEZEKANA KUTOKA TIGO KUPITIA TIGO JIHUDUMIE)
Kampuni ya simu ya Tigo imeanzisha huduma inayoitwa JIHUDUMIE ambayo itamsaidia mteja aliyetuma muamala wa fedha kimakosa kuweza kurejesha fedha zake kwa njia rahisi na haraka zaidi.
Mteja akikosea kutuma pesa hahitaji msaada wa moja kwa moja kutoka kitengo cha huduma kwa wateja bali atapiga menyu ya Tigo pesa (*150*01#) kisha atachagua huduma ya Jihudumie na kufuata maelekezo yatakayojitokeza kuwezesha kurudisha muamala wake.
Kwa sasa Mteja ataweza kurejesha miamala ya tigo kwenda tigo.

kama una mawsali zaidi juu ya Huduma hii mpya toka tigo acha comments zako apo chini 

Thursday 17 May 2018

FAHAMU TEAMVIEWER NA VIPI INAWEZA KUOKOA SIKU YAKO

Wadau leo tutapata maujanja ya software moja ambayo inaweza kuokoa sana siku yako.


TeamViewer

Hii ni software ambayo inaweza kurahisisha sana maisha haswa kwa watu wa technical kwa kuwa software hii inaweza kufanya kitu kinaitwa (remote access) yaani uwezo wa ku control computer moja kwa kutumia computer nyingine ukiwa mbali nayo. (mfano kama uko na computer dar es salaam na wewe uko ata kama UK unachofanya una install software kwenye computer yako na kwenye computer upande wa pili pia software iwe installed.
pia software hii inafanya kazi kwenye vifaa vingine kama tablets na smart phones ivyo una uwezo wa ku access computer iliyo mbali ata kwa kutumia smartphone ana tablet yako. 

kwa watu wa technical mnaweza kusaidiana kitu kama mtu amekwama na wewe ndio expert ya kitu hicho, nyote mta fungua team viewer na utaweza ku access desktop ya Rafiki yako na kum assist safi kabisa kama vile uko eneo hilo
(mnaweza ku chatt kwa msg ama video na Rafiki unae mu assist live)

kwa watu wa kawaida unaweza kuwa  umesahau files zako muhimu kwenye computer yako na umesafili  bila computer na utaitaji izo file utaweza kuzipata, team viewer ndio njia pekee rahisi kwani ukitumia software hii kama kawaida utaweza ku access desktop yako ikiwa ni pamoja na kuperuzi computer yako kwa  kokote utakako na ku copy file lako muhimu ki lainiiii ata kwa kutumia tu tab au smartphone yako
(hakuna tena presha ya kuwa umesahau file muhimu maujanja ni team viewer)


cha kuzingatia wakati wa installation uchague option ya personal ili kutumua free  

cheki apa kupakua software hiyo
kwa kifaa smart device yako ingia kwa store yako na pakua bure kabisa

Wednesday 16 May 2018

KU RESTORE MAC YAKO KWA INTERNET IKIWA IMEKUFA AU UMEBADILI HDD MPYA

leo tutapata maujanja jinsi gani ya kurekebisha mac yako na kuirudisha kuwa safi (format) kwa internet. 
njia hii ni njia nzuri sana na salama zaidi ya ku restore mac yako, njia hii itapunguza hekaheka njingi unazoweza kupata ukitumia njia nyingine ku restore.
utatakiwa kuwa na internet enye kwenda vizuri bila ku kata kata (stable) na pia uwe na bundle sio chini ya 5gb 


JINSI YA KUANZA 
Utawasha mac yako na kwa kutumia keyboard yako utabonya key 3 kwa pamoja ukiwa unawasha mac yako (option command + ) 

ukiwa umebonya izo key 3 kwa pamoja moja kwa moja utapelekwa kwenye recovery mode 
utaendelea kufuata muongozo kutoka kwenye screen yako 
apa utachagua wireless yako na kuweka password zako kama zipo


hatua hii ndipo umakini unapotakiwa zaidi kwa kuwa unataka ku restore mac yako na kuwa fresh kabisa kama mpya, utatakiwa kwanza uende kwenye disk utility ili ku format kabisa ndipo urudi kwenye re install os x, ukianza na reinstall osx moja kwa moja utaweza kupata errs zitakazokupa changamoto 

Ndani ya disk utility utafuta data tayari kwa kuanza reinstallation ya os x 
baada ya apa utarudi nyuma na kuendelea na installation na mac os x kwenye mashine yako, fuatiza tu miongozo inayotoka kwenye kioo mpaka unapimaliza kufanya restore mac yako. 
mpaka hapo utakuwa ushamaliza ku restore mac yako na itakuwa safi kama mpya. enjoy
kama una swali tafathali comment apo chini 

Sunday 13 May 2018

KU INSTALL WINDOWS BILA KUPOTEZA DATA ZAKO

Changamoto hii tunaipata mara nyingi sana pale computer zetu zinapokuwa zime pata tatizo ambapo inalazimika ku install windows upya (kupiga chini) lakini unabaini kwamba kwnye computer yako kuna data muhimu ambazo hazitakiwi kupotea.

Leo tutapata maujanja njia mbili tofauti unazoweza kutumia katika kufanya installation bila kupoteza data zako muhimu kwenye computer.

NJIA YA KWANZA 
Ni kwa kutumia software ambozo zinaweza kuwasha computer yako kutoka kwekye flash ama cd bila ku install kwenye computer (live cd software) mfano. ububtu / Hiren's: Boot CD na nyinginezo.  
Hapa utawekamojawapo ya software izo kwenye flash yako ama uta andika kwenye cd yako na kisha uta washa mashine na kama kawaida kwa kutumia bios yako utafanya setting kwamba computer ianze kuwaka kutoka kwa flash ama cdrom yako kutegemea hiyo software yako umeweka wapi.
Kisha computer yako kuisoma ile software kwenye flash/ ama cd yako itawaka na kukupa muda wa kufanya backup ya data zako zote muhimu na baada ya apo ndipo uanze hatua ya ku install window yako.

NJIA YA PILI 
Hapa hakuna software yoyote ya pembeni utakayotumia, utatakiwa tu kuwa makini wakati wa istallation usiweze kupoteza data zako. utakachokifanya hapa ni kama kawaida utakuwa na cd yako ya windows ana kama ulishatengeneza flash yako ya window, utaweka kwenye computer yako na kufanya setting za bios kwamba computer ianze kuwaka toka kwa flash ama kwa cd yako ya window.
Kama kawaida computer ikishasoma cd ama flash yako itaweza kuwaka ikianza kukuletea hatua za installation kama kawaida.

Sasa hapa ndipo umakini unapotakiwa usiweze kupoteza data zako, utafuata muongozo kama ifuatavyo. haijalishi kama ulikuwa na window ya chini unataka ku install ya juu (mfano 7 na unataka 8 ama 10) ama unataka kurudisha window yako uliyokuwa nayo. - kwa wale walio na windowa 10 kuna njia nzuri zaidi ambayo haipotezi data inajulikana kama refresh.
(miongozo inafanana kwa windows zote apa utapata mfano kwa windows 7)
kama nilivyoeleza mwanzo ukiwa tayari umeshaandaa window cd ama flash yako na umesha fanya setting za bios kulingana kitu gani utatumia ku unstall window yako.
washa computer ukiwa umeshaweka cd ama kuchomeka flash
computer itasoma chanzo chako cha installation ka kukuletea miongozo ka ifuatavyo 


Hapa ndio installation inaanza utasubiri 
utachagua lugha alafu utabonya next 
apa utakubali terms  za Microsoft alafu bonya next 
apa utachagua option ya custom(advance) na sio upgrade 
sasa apa ndipo umakini zaidi unapoitajika utachagua partition ile ile ambayo ilikuwa na windows yako ya awali, bila kufanya format (narudia tena kwa msisistizo usifanye format) na ukibonya tu next upata jumbe kwamba partition uliochagua tayari ina window na itakuwa saved kwenye folder linaoitwa "old windows", kubaliana na hilo kisha endelea.
hapa utasubiri installation imalize kazi na mwisho kabisa baada ya kila kitu kukamilika utaweza kupata datazako zote zikiwa safi kwenye folder linalopatikana kwenye drive c: linaitwa old windows 
ukifungua old windows folder utakuta folders nyingine nenda kwenye users folder na tafuta jina ulilokua utatumia kwenye computer kabla ya kupata shida umo utakuta data zako zote salama salmin.

Mpaka hapo utakuwa umemaliza zoezi, kama una sawali ama unaitaji maelezo tuachie comment yako apo chini.

Wednesday 9 May 2018

NINI CHA KUFANYA UKIPATA ERROR WAKATI WA KU RESTORE/UPDATE IPHONE, IPAD AU iPOD

Tumekua kunapata error za aina mbali mbali wakati tukiwa tuna restore / update iphone, ipad, na apod zetu bila kubaini nini hasa kisababishi. 
leo tutapata dondoo kwamba nini cha kuangalia kwanza ukiwa unapata error wakati una update/restore iphoe,ipad,apod yako. 

MAMBO YA KUANGALIA 

1. utahakikisha utatumia itune version mpya kabisa (pata latest version hapa)  
2. hakikisha ume update operation system yako (windows/mac)

3. Tumia cable original na uchomeke moja kwa kwenye computer yako usitumie HUB ama connector ya aina yoyote.

4. Zima computer yako pamoja na device yako alafu washa tena
5. Angalia security software kwenye computer yako maana ziko software nyingine zinazoweza ku kinzana na connection kati ya computer itune na device ivyo unaweza kulazimika ku disable ama ku unistall security software husika kwanza. (security softwarezinazotengenezwa na kampuni nyingine tofauti na apple zinaweza kuzuia itune kuwasiliana na apple servers au devices)
6. jaribu tena ku restore/update device
kwa swali lolote Tafadhali comment apo chini 

Tuesday 8 May 2018

JINSI YA KU INSTALL NORTON SECURITY MPYA

Norton security ni latest computer software security suite iliyotolewa na wakongwe symentic. inafanya kazi na ms windows, mac os x, android, and ios platforms. zinapatikana kwa editions 3, norton security standard, norton security deluxe, na norton security premium.
norton security standard kwa 1 device, norton security deluxe kwa 5 devices, na norton security premium kwa mpaka 10 devices.
pia zinapatikana kwa (special editions)
NAMNA YA KUFANYA INSTALLATION 

unaweza ku install kwa online ama kutoka kwa cd uliyonunua kutoka kwa dealer (tucheki computerdevicedr 0767240679- tunazo kwa bei nafuu sana)
https://computerdevicedr.wixsite.com/tanzania/shop

tunaanzan na ku install kutoka kwenye cd moja kwa moja, utaweka cd ya norton security kwenye computer yako, na baada ya muda kidogo kawa kawaida ya installations tulivyozoea ita pop window ambayo ita ku guide kwenye installation nzima. 
Hatua ya mwishoni utapata muongozo wa ku log in na norton account kama huna utatakiwa kufungua norton account mpya. 


Apa utajiuliza kwa nini ufungue account?...... account ya norton security ina msaada mkubwa sana kwenye installation za norton security pale ambapo una install kwenye device zaidi ya moja. 
Pia itakusaidia endapo device yako imepata shida ukaitaji ufanye installation upya norton security ata kama umesahau/umepoteza KEY ukiwa na account ya norton security uki log in umemaliza kila kitu kinajiweka sawa.

Si ivyo tu pia ukuwa una install device zaidi ya moja na una KEY ya device zaidi ya moja pia uki log in tu kwa norton security kutumia na accounti yako wakati una install device nyingine kila kitu kinakuwa activated automatically.

Nilichopenda zaidi ni kwamba mfano kama ume install kwenye computer yako  ya home na umesafiri ghafla na laptop yako na hautaki ku risk lakini hujapata mda wa kununua norton security fasta fasta kwenye laptop, unaweza uka download kutoka  internet alafu uka log in kwa ile account ya computer yako ya home na fasta utapewa option kama unataka kuamisha license na ukikubali laptop inakuwa full activated kutumia licence ya kwenye computer ya home na Maisha yanaenda saaaafiii😎😎😎😎😋….. norton aisee chiboko kweli mkongwe mkongwe tu.

kwa installation ya  kwenye mobile device utaingia kwenye app store yako na ku download norton security   kisha install na utamaliza kwa kuweka key ambayo umepata wakati wa kunua. 
mpaka apo. utakuwa umeshamaliza installation yako. kama hko na sawali acha comment yako apo chini.